Swali: Tumepata Hadiyth kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mtu anaweza hufanya matendo ya watu watu wa kheri kwa miaka sabini, lakini anapoweka wasia na akafanya (حاف) katika wasia wake, basi mwisho wake unakuwa ni mbaya na anaingia Motoni.”

Nini maana ya neno (حاف)?

Jibu: Yamekuja katika Hadiyth nyingi za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) maana inayofanana na hii kutoka kwa Ibn Mas’ud (Radhiya Allaahu ´anh) aliyoipokea al-Bukhaariy na Muslim na Hadiyth nyingine: kwamba mja anatenda matendo ya watu wa Pepo mpaka kusibaki baina yake na Pepo isipokuwa dhiraa moja, kisha yamtangulie yaliyoandikwa ambapo atatenda matendo ya watu wa Motoni na kuingia akaingia Motoni. Kwa maana ya kwamba anatokewa na mwisho mbaya. Imekuja katika baadhi ya riwaya:

”Hakika mja anatenda matendo ya watu wa Pepo kwa yale yanayoonekana kwa watu.”

Kwa maana kwa dhahiri ya hali yake. Kisha katika mwisho wa maisha yake anatenda matendo ya watu wa Motoni na akaingia Motoni. Hakika mja anatenda matendo ya watu wa Motoni kwa yale yanayoonekana kwa watu, kisha katika mwisho wa maisha yake anatenda matendo ya watu wa Pepo ambapo Allaah anamkubalia tawbah yake na hivyo akaingia Pepo. Matendo yanazingatiwa mwisho wake.

Neno (حاف) katika wasia ni mtu kuusia kwa kile kisichomfaa, kwa mfano kuusia mrithi, ilihali mrithi hana wasia. Yanawatosha yale ambayo Allaah (Ta´ala) amewapangia:

”Hakika Allaah amempa kila mwenye haki haki yake, hivyo basi hakuna wasia kwa mrithi.”

Neno (حاف) katika wasia ni mtu kuzidisha zaidi ya thuluthi bila idhini ya warithi au kuwausia baadhi ya warithi, jambo ambalo halijuzu. Ni wajibu wake kujizuia katika thuluthi au chini yake na asimuusie mrithi yeyote.

Ama kuhusu Hadiyth hii, mimi sijui hali ya cheni yake ya wapokezi. Inahitaji kuchunguzwa cheni yake ya wapokezi. Lakini maana yake ni kwamba mtu akifanya maovu mwishoni mwa maisha yake, akafanya maasi na akafa juu ya hayo, basi kunakhofiwa kuingia Motoni kwa sababu ya mwisho mbaya.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1131/المراد-بالحيف-في-الوصية
  • Imechapishwa: 17/08/2026