Kuna hekima gani ya kuanza kisimamo cha usiku kw Rak´ah mbili fupi?

Swali: Kuna hekima gani ya kuanza kisimamo cha usiku kwa Rak´ah mbili nyepesi?

Jibu: Allaah ndiye anayejua zaidi. Lakini huenda hekima yake ni kumwandaa mswaliji kwa muda mrefu wa kusoma Qur-aan na kufanya Rukuu´. Kwa maana nyingine kunamtia nguvu. Kwa sababu pengine yuko na udhaifu fulani. Kwa hivyo akiswali Rak´ah mbili fupi basi kumtia moyo na kumwandaa kwa swalah ndefu zinazofuata – na Allaah ndiye mjuzi zaidi. Hata hivyo sina maandiko ya moja kwa moja kuhusu hili, lakini inawezekana kuwa hii ndiyo sababu sahihi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24881/ما-الحكمة-في-استفتاح-القيام-بركعتين-خفيفتين
  • Imechapishwa: 26/12/2024