Kuna fadhilah zozote za kuhiji siku ya ijumaa?

Swali 28: Je, limekuja jambo lolote kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu ubora wa kuhiji siku ya ijumaa?

Jibu: Haikupokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu ubora wa ijumaa ikiwa itakutana na siku ya ´Arafah. Lakini wanazuoni wanasema kwamba kukutana kwake na siku ya ijumaa ndani yake kuna kheri:

1 – Ili Hajj yake iwe kama Hajj ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kusimama kwake ´Arafah kuliafikiana na siku ya ijumaa.

2 – Hakika katika siku ya ijumaa kuna saa ambayo mja muislamu hakutani nayo akiwa amesimama anaswali akimuomba Allaah kitu isipokuwa Allaah humpa kitu hicho. Hivyo inakuwa hiyo ni karibu zaidi na kujibiwa.

3 – Siku ya ´Arafah na ijumaa zote ni sikukuu. Kwa hivyo ikiwa sikukuu hizo mbili zitaafikiana basi hilo linakuwa na kheri.

Hata hivyo kuhusu yale yaliyoenea kwamba kufanya Hajj siku ya ijumaa ni sawa na Hajj sabini si sahihi.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/35)
  • Imechapishwa: 07/05/2026