Swali: Kuna dhambi kwa mwanamke kutumia rangi ya kucha inayotiwa katika kucha? Afanye nini wakati anapotawadha?
Jibu: Hatujui chochote juu ya hili. Lakini bora ni kutofanya hivo kwa sababu hakuna haja ya jambo hilo. Jengine ni kwamba inaweza kuzuia maji kufika kwenye ngozi wakati wa kutawadha. Kwa kuhitimisha ni kwamba bora ni kutofanya hivo na mtu atosheke na hina. Bora ni kushiamana na yale waliokuwa nayo watu wa mwanzo. Mwanamke akiitumia basi ni lazima aiondoshe wakati wa kutawadha. Kwa sababu kama tulivyotangulia kusema inazuia maji kufika kwenye ngozi.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/48)
- Imechapishwa: 06/08/2021
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Ni ipi hukumu ya wudhuu´ wa mwanamke aliyepaka rangi ya kucha?
Swali: Ni ipi hukumu ya wudhuu´ kwa yule ambaye kwenye kucha zake amepaka rangi ya kucha? Jibu: Rangi ya kucha ni kitu anachopaka mwanamke juu ya kucha na ni kitu kilicho na ukoko. Haijuzu kwa mwanamke kuitumia kipindi ambapo anaswali kwa kuwa inazuia maji kufika kwenye ngozi wakati wa kutawadha.…
In "Wudhuu´"
Kurefusha kucha ni kujifananisha na wanyama na makafiri
Swali: Ni ipi hukumu ya kurefusha kucha na kuweka juu yake rangi ya kucha pamoja na kuzingatia kwamba hutawadha kabla ya kuiweka na hukaa masaa 24 kisha naiondosha? Jibu: Kurefusha kucha ni jambo linaenda kinyume na Sunnah. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amesema: “Mambo ya…
In "Kucha"
Josho la janaba na wudhuu´ wa ambaye amefunga bendeji au amepaka rangi ya kucha
Swali: Je, inasihi kuoga janaba ikiwa vidole vina rangi ya kucha? Jibu: Ikiwa kuna kitu juu yake kinapaswa kuondolewa - ni mamoja rangi ya kicha au vinginevyo - vitu vilivyobandikwa ambavyo ni mchezo na visivyo na haja, hivyo vinaondolewa. Lakini bandeji, hupitisha juu yake maji. Lakini ikiwa ni rangi ya…
In "Josho la janaba"