Kuna aina mbalimbali ya kupangusa kichwa

Swali: Kufuta kichwa inakuwa mara moja bila kurudisha mikono?

Jibu: Si lazima. Kumepokelewa aina mbalimbali katika kufuta kichwa. Muhimu ni kufuta kichwa na inatosha, ni mamoja iwe amerudisha mikono au hakurudisha, au ameanza katikati ya kichwa akaenda hadi nyuma kisha mbele, jambo hili ni lenye wasaa. Lakini kilicho bora ni kuanza mbele ya kichwa, kisha aende hadi nyuma, halafu arudi tena mbele. Hilo ndilo bora zaidi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31519/حكم-مسح-الراس-في-الوضوء-بدون-ارجاع
  • Imechapishwa: 31/10/2025