Swali: Ni ipi hukumu ya kumzika maiti ndani ya msikiti na kuufanya kuwa mahali pa kuzuriwa na kupata fedha kupitia hilo?

Jibu: Hili ni jambo la maovu. Haijuzu kumzika maiti ndani ya misikiti. Misikiti si makaburi, bali wafu huzikwa nje ya misikiti, katika maeneo maalum kama makaburini au jangwani. Wala haijuzu kujenga msikiti juu ya kaburi na wala kumzika mtu ndani ya msikiti. Mambo yote mawili ni haramu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah amewalaani mayahudi na manaswara. Wameyafanya makaburi ya Mitume wao kuwa misikiti. Zindukeni! Hakika wale waliokuwa kabla yenu walikuwa wakiyafanya makaburi ya Mitume wao na waja wao wema kuwa misikiti. Zindukeni! Msiyafanye makaburi kuwa misikiti. Hakika mimi nawakatazeni kutokana na hilo.”

Hivyo watu wanapaswa kunasihiana na kufundishana. Ikiwa mtu amezikwa ndani ya msikiti, basi kaburi hilo linapaswa kufukuliwa na maiti kuhamishwa kwenda makaburini. Haijuzu kuiacha kaburi ndani ya msikiti. Tunamuomba Allaah atuongoze.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3416/حكم-دفن-الموتى-في-المساجد-واتخاذها-قبورا
  • Imechapishwa: 22/08/2026