Swali: Mwanaume alimtaliki mke wake mwaka mmoja uliopita kwa talaka moja na wana watoto. Mwanamke bado anaishi karibu na nyumba ya mume wake pamoja na watoto na nyumba ni ya mume. Je, inajuzu kwa mwanaume kumrudia mke wake bila kupitia mahakama au kwa hakimu?
Jibu: Ikiwa alimtaliki talaka moja tu na haikutanguliwa na talaka nyingine, basi anaweza kumrejea muda wa kuwa bado yuko ndani ya eda. Ikiwa tayari ametoka katika eda – kama ilivyotajwa – basi inabidi amuoe tena kwa ndoa mpya pamoja na walii wake. Walii wake ni wa karibu zaidi katika upande wa jamaa zake baba. Ikiwa ana baba, ndiye anayemuozesha. Ikiwa hana baba, basi babu yake. Ikiwa ana mtoto wa kiume mkubwa na mwenye akili timamu, anaweza kumuozesha. Ikiwa hakuna hao, basi ndugu yake wa baba na mama, kisha ndugu wa baba, kisha wana wa ndugu na hivyo hivyo kwa mpangilio wa jamaa wa upande wa baba wa karibu zaidi. Ikiwa jambo hili litamshangaza au kumchanganya, basi aulize wanazuoni katika nchi yake ili waelekezwe.
Kwa kumalizia hakuna ulazima wa kwenda kwa hakimu au mahakama ikiwa mwanamke ameridhia na walii wake amemuozesha, basi hakuna tatizo. Talaka moja au mbili hazimharamishi mke kwake. Kinachomharamisha kabisa ni talaka ya tatu. Kwa hiyo ikiwa eda imekwisha, anaweza kumuoa tena kwa ndoa mpya, kwa walii wake na kwa mahari watakayokubaliana, hata kama ni kidogo, kama pesa moja au kiasi kingine chochote watakachokubaliana.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3429/حكم-مراجعة-المطلقة-رجعيا-بعد-انقضاء-عدتها
- Imechapishwa: 22/08/2026
Swali: Mwanaume alimtaliki mke wake mwaka mmoja uliopita kwa talaka moja na wana watoto. Mwanamke bado anaishi karibu na nyumba ya mume wake pamoja na watoto na nyumba ni ya mume. Je, inajuzu kwa mwanaume kumrudia mke wake bila kupitia mahakama au kwa hakimu?
Jibu: Ikiwa alimtaliki talaka moja tu na haikutanguliwa na talaka nyingine, basi anaweza kumrejea muda wa kuwa bado yuko ndani ya eda. Ikiwa tayari ametoka katika eda – kama ilivyotajwa – basi inabidi amuoe tena kwa ndoa mpya pamoja na walii wake. Walii wake ni wa karibu zaidi katika upande wa jamaa zake baba. Ikiwa ana baba, ndiye anayemuozesha. Ikiwa hana baba, basi babu yake. Ikiwa ana mtoto wa kiume mkubwa na mwenye akili timamu, anaweza kumuozesha. Ikiwa hakuna hao, basi ndugu yake wa baba na mama, kisha ndugu wa baba, kisha wana wa ndugu na hivyo hivyo kwa mpangilio wa jamaa wa upande wa baba wa karibu zaidi. Ikiwa jambo hili litamshangaza au kumchanganya, basi aulize wanazuoni katika nchi yake ili waelekezwe.
Kwa kumalizia hakuna ulazima wa kwenda kwa hakimu au mahakama ikiwa mwanamke ameridhia na walii wake amemuozesha, basi hakuna tatizo. Talaka moja au mbili hazimharamishi mke kwake. Kinachomharamisha kabisa ni talaka ya tatu. Kwa hiyo ikiwa eda imekwisha, anaweza kumuoa tena kwa ndoa mpya, kwa walii wake na kwa mahari watakayokubaliana, hata kama ni kidogo, kama pesa moja au kiasi kingine chochote watakachokubaliana.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3429/حكم-مراجعة-المطلقة-رجعيا-بعد-انقضاء-عدتها
Imechapishwa: 22/08/2026
https://firqatunnajia.com/ni-lazima-mwanaume-kwenda-kwa-hakimu-wakati-wa-kumrejea-mke-wake/