Swali: Inajuzu kumwita mtu ´bwana wangu`?

Jibu: Kusema ´bwana wangu` ni jambo sahali. Lakini hata hivyo kuliacha ndio bora zaidi. Lakini kusema ´bwana wangu` haina neno. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika mwana wangu huu ni bwana.” al-Bukhaariy (2704).

Akimaanisha al-Husayn. Vilevile alikuwa akiuliza kuhusu wale wakuu wa makabila ni nani ambaye ni bwana wa wana fulani. Ni nani bwana wa wana fulani? Anasema hivo akimaanisha mkuu wao. Vilevile alimwambia Sa´d bin Mu´aadh:

“Simameni kwa ajili ya bwana wenu.”

Pindi alipokuja kuwahukumu Banuu Quraydwah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 27
  • Imechapishwa: 02/11/2016