Swali: Kumwita mtu aliyekulea “Baba” kwa njia ya kumuheshimu.

Jibu: Kujinasibisha kwa asiyekuwa baba yako ni dhambi kubwa. Haifai kwake kuleta msemo huu. Kwa sababu inafanana na yule mwenye kujinasibisha kwa asiyekuwa baba yake.

Ama akisema hivi kwa njia ya kumuadhimisha na kumheshimu, kama jinsi anavomwambia mtu mzima “ee baba yangu”, “ee ami” au kama anavomwambia mwanachuoni “ee baba” na mfano wa hivo – kwa njia ya heshima – haina neno Allaah akitaka.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (27) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1428-4-13.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020