Swali: Ni ipi hukumu ya kumvuta mswaliji anayeswali katika safu ya mbele ili aswali pamoja nami katika safu ya nyuma?

Jibu: Haifai kufanya hivo kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi. Jaribu ujipenyeze ndani ya safu ukiweza kufanya hivo. Vinginevyo subiri mpaka pale atakapokuja mtu ambapo utapanga naye safu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (30)
  • Imechapishwa: 20/02/2022