Kumuuzia mtu mnyama na baadaye kugawana faida yake

Swali: Je, inafaa kumpa mtu ng´ombe au kondoo kwa thamani ndogo kisha nikamwambia amlishe mnyama huyo mpaka akuwe mkubwa na kunenepa na kwamba tutagawana ile faida yenye kuzidi juu ya ile thamani tuliyokubaliana?

Jibu: Hilo ni jambo zuri na halina neno. Akifa khasara inakuwa kwa wote wawili. Faida na khasara inakuwa kwa wote wawili.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 291
  • Imechapishwa: 09/01/2025