Kumuombea ndugu aliyekufa katika shirki kuwepesishiwa adhabu

Swali: Ni jambo lenye kujulikana kwamba haijuzu kuwaombea du´aa washirikina wanapokufa katika shirki. Je, inajuzu kwa ndugu ambaye amekufa juu ya shirki kumuombea du´aa Allaah amkhafifishie adhabu tu bila ya kumuombea du´aa ya msamaha, kwa mfano akaomba kwa kusema “Ee Allaah mkhafifishie adhabu”?

Jibu:

مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ

“Haimpasi Nabii na wale walioamini kuwaombea msamaha washirikina japokuwa ni jamaa zao wa karibu baada ya kuwabainikia kwamba wao ni watu wa Motoni.” (09:113)

Hata kama itakuwa ni baba yako au mwanao haijuzu kumuombea baada ya kufa kwake wala msamaha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (54) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-11-03.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020