Kumuomba Allaah Pepo na kukingwa na Moto ndani ya swalah

Swali: Je, inafaa kwa mswaliji wakati anapopita kwenye kisomo chake kutaja Pepo na Moto akamuomba Allaah amwingize Peponi na akamuomba amkinga kutokamana na Moto? Je, katika hilo ipo tofauti kati ya maamuma na mtu anayeswali peke yake?

Jibu: Ndio, inafaa kufanya hivo. Hakuna tofauti kati ya imamu, anayeswali peke yake na maamuma. Isipokuwa tu kwa maamuma imewekwa sharti jambo hilo lisimshughulishe kunyamaza ambako yeye ameamrishwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Arkaan-il-Islaam, uk. 344
  • Imechapishwa: 09/05/2020