Kumuoa mwanamke ambaye mtu amembebesha mimba

Swali: Kuna mtu amezini na mwanamke na akambebesha mimba. Je, inajuzu kwake kumuoa na inahesabika mimba hii ni yake?

Jibu: Hapana. Mimba sio yake. Mtoto ni wa kitandani na huyu sio wa kitandani. Huyu ni mtoto wa nje ya ndoa na hivyo atanasibishwa kwa mama yake.

Ama kuhusu kumuoa, wote wawili wakitubia Tawbah sahihi, anaweza kumuoa yeye au mwengine. Wakitubia wote wawili Tawbah sahihi, hakuna neno wakaoana.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14221
  • Imechapishwa: 17/11/2014