Kumuitikia muadhini ndani ya swalah

Swali: Je, inajuzu kumjibu muadhini wakati mtu anaposwali swalah ya sunnah?

Jibu: Hapana. Anayeswali, ni mamoja swalah ya faradhi au sunnah, asimjibu muadhini. Ni mwenye kushughulishwa na swalah. Atekeleze swalah ambayo yuko anaswali.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (31) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1430-10-9.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020