Swali: Tunasikia na kusoma katika vyombo vya khabari kwamba kumpiga mwanamke ni njia isiyokuwa sahihi, kwamba haisaidii kitu, kwamba ni kitendo cha unyama na kwamba ni jambo linaongeza tu matatizo ya kindoa. Je, huku ni kuchukia yale aliyoteremsha Allaah?
Jibu: Ndio. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:
وَاللَّاتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ
“Na wale ambao mnachelea uasi wao wa ndoa, basi wanasihini na wahameni katika malazi na wapigeni.” (04:34)
Amefanya kumpiga mke ni aina moja wapo ya kumtia adabu. Lakini inahusu kipigo kisichoumiza. Anayesema kuwa kumpiga mwanamke ni uovu amepingana na hukumu ya Allaah (Ta´ala). Anayesema kuwa adhabu zilizowekwa katika Shari´ah ni za unyama kama vile kukata mkono wa mwizi, kumpiga mzinifu ambaye kishaingia katika ndoa na kadhalika, hapana shaka kwamba amepingana na hukumu za Allaah (´Azza wa Jall). Kukataa hukumu ya Allaah ni kufuru.
Ikiwa huyu anapinga ule msingi wa kumpiga mwanamke basi amekataa kitu kilichowekwa na Allaah (´Azza wa Jall). Ama ikiwa kupinga kwake anamaanisha kwamba kupiga iwe hatua ya mwisho na kwamba mtu asikimbilie kupiga tu, lakini mtu aanze kufanya zile hatua zengine kwanza kisha aende hatua kwa hatua au anamaanisha kwamba mtu asimpige kipigo cha sana, huyu kuna ukweli fulani katika maneno yake. Kila jambo linawekwa mahala pake. Kipigo kinatakiwa kuwekwa mahala pake alipopaweka Allaah (Ta´ala). Haitakiwi kupiga katika kila jambo.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam https://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/04.mp3
- Imechapishwa: 01/12/2018
Swali: Tunasikia na kusoma katika vyombo vya khabari kwamba kumpiga mwanamke ni njia isiyokuwa sahihi, kwamba haisaidii kitu, kwamba ni kitendo cha unyama na kwamba ni jambo linaongeza tu matatizo ya kindoa. Je, huku ni kuchukia yale aliyoteremsha Allaah?
Jibu: Ndio. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:
وَاللَّاتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ
“Na wale ambao mnachelea uasi wao wa ndoa, basi wanasihini na wahameni katika malazi na wapigeni.” (04:34)
Amefanya kumpiga mke ni aina moja wapo ya kumtia adabu. Lakini inahusu kipigo kisichoumiza. Anayesema kuwa kumpiga mwanamke ni uovu amepingana na hukumu ya Allaah (Ta´ala). Anayesema kuwa adhabu zilizowekwa katika Shari´ah ni za unyama kama vile kukata mkono wa mwizi, kumpiga mzinifu ambaye kishaingia katika ndoa na kadhalika, hapana shaka kwamba amepingana na hukumu za Allaah (´Azza wa Jall). Kukataa hukumu ya Allaah ni kufuru.
Ikiwa huyu anapinga ule msingi wa kumpiga mwanamke basi amekataa kitu kilichowekwa na Allaah (´Azza wa Jall). Ama ikiwa kupinga kwake anamaanisha kwamba kupiga iwe hatua ya mwisho na kwamba mtu asikimbilie kupiga tu, lakini mtu aanze kufanya zile hatua zengine kwanza kisha aende hatua kwa hatua au anamaanisha kwamba mtu asimpige kipigo cha sana, huyu kuna ukweli fulani katika maneno yake. Kila jambo linawekwa mahala pake. Kipigo kinatakiwa kuwekwa mahala pake alipopaweka Allaah (Ta´ala). Haitakiwi kupiga katika kila jambo.
Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam https://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/04.mp3
Imechapishwa: 01/12/2018
https://firqatunnajia.com/kumtia-mwanamke-adabu-haifai-na-ni-unyama/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)