Kumtanguliza nduguyo katika mambo ya ´ibaadah

Swali: Ni upi usahihi wa maneno yanayosema:

“Hakuna kupendeleana katika ´ibaadah”?

Jibu: Maneno haya yamesemwa na baadhi ya wanachuoni. Baadhi ya wanachuoni wanaona kuwa kupendeleana kunakuwa katika mambo ya kidunia. Ama katika mambo ya ´ibaadah hakuna kupendeleana. Ni kama kwa mfano mtu akajitolea juu ya nafsi yake na akamtanguliza nafasi yake katika safu na ukamtanguliza yeye katika kitu katika ´ibaadah na matendo mema. Wanachuoni wengine wanaona kuwa hakuna neno mtu akampendelea mwengine katika ´ibaadah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (13) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191589#219913
  • Imechapishwa: 18/10/2019