Swali: Je, inafaa kusema ”Faatwimah, amani iwe juu yake.”?

Jibu: Hapana vibaya. Hata hivyo kusema ”Radhi za Allaah ziwe juu yake” ndio bora kama ilivyo kwa Maswahabah wengine. Hata hivyo hapana vibaya mtu akisema ”amani iwe juu yake, juu ya ´Aliy, juu ya ´Uthmaan, juu ya as-Swiddiyq au juu ya ´Umar. Lakini mtu asichukulie ndio nembo kwa baadhi ya watu pasi na wengine. Bora katika hali hii ni kuwatakia radhi ili baadhi yao wasifanywe kuwa maalum na hilo likawapelekea katika kuchupa mipaka. Hata hivyo ni sawa mtu akisema hivo baadhi ya nyakati bila ya kuendelea na jambo hilo na kuchukulia ndio nembo kwa baadhi badala ya wengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24274/هل-يجوزقول-عليها-السلام-لفاطمة
  • Imechapishwa: 26/09/2024