Swali: Utukufu wa Madiynah kama utukufu wa Makkah kunajumuisha makafiri kuingia ndani yake?

Jibu: Haya ni miongoni mwa yale ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alibainisha katika Hadiyth ya Makkah na kuharamishwa kuwalinda hapo… kuhusu kuingia washirikina jambo haliko wazi, kwa sababu yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwakubalia washirikina kuingia. Ujumbe wa Najraan na manaswara waliingia kwake. Ujumbe wa Thaqiyf pia walikuwa washirikina. Kwa hivyo udhahiri wa Hadiyth ni kwamba Madiynah sio kama Makkah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24299ما-حكم-دخول-المشركين-الى-المدينة
  • Imechapishwa: 26/09/2024