Kumsubiri arudie imamu aliyetoka ndani ya swalah

Swali:  Je, bora kwa imamu aseme ´subirini!` au ateue mtu mwingine mahali pake?

Jibu: Bora awaambie ´bakieni mahala penu mpaka nirejee!` ikiwa mahali pake ni karibu na hawatii uzito. Vinginevyo atateua mwingine ambaye atawaswalisha.

Swali: Matukio ya Hadiyth hii ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema:

“Bakieni mahali penu!”

Imekuja katika baadhi ya matamshi:

“… baada ya kuleta Takbiyr.”

Kisha akarudi na kujiunga na swalah na wala hakurudia tena Takbiyrat-ul-Ihraam?

Jibu: Haya ni matukio mengine. Arudi na awakamilishie swalah yao, kwa sababu wamekwishapiga Takbiyr baada yake ambayo walifikiria kuwa yuko na twahara.

Swali: Lakini akirudia Takbiyr yake inakuwa baada ya Takbiyr yao?

Jibu: Ndio, Takbiyr yao kwa nisba ya Takbiyr yake ya kwanza iliyotangulia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23713/هل-يشرع-انتظار-الامام-لعارض-حتى-يرجع
  • Imechapishwa: 12/04/2024