Kumsalimia mwanamke asiye Mahram nyuma ya kitambaa

Swali: Je, inajuzu wakati wa kumsalimia mwanamke mwanaume kuweka kitambaa mkononi mwake au mwanamke naye aweke kitambaa mkononi mwake kisha wasalimiane kwa kushikana mikono?

Jibu: Haifia kusalimiana kwa kushikana mikono na wanawake. Bali unasalimia kwa maneno tu bila ya kushikana mikono, si kwa kuweka kitambaa wala bila kitambaa. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mimi sisalimiani kwa kushikana mikono na wanawake.”

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3181/حكم-مصافحة-النساء-من-وراء-حاىل
  • Imechapishwa: 01/08/2026