Zakaah inatolewa juu ya mtaji na faida zake

Swali: Kuna mradi mdogo wa mifugo. Mimi nina mtaji na mwingine anatoa juhudi na faida inagawanywa nusu kwa nusu. Ni ipi hukumu ya zakaah katika hali hii? Ikiwa mnyama atakufa, je, inapunguzwa katika mtaji wa msingi au katika faida?

Jibu: Zakaah inatolewa juu ya fedha zilizopo na juu ya mifugo ikiwa ni ya biashara na kuuza. Hivyo mifugo inatolewa zakaah na pia fedha zote zilizokusanywa – mtaji na faida zake – zote zinatolewa zakaah. Ikiwa baadhi ya mifugo itakufa, basi hasara hiyo inahesabiwa juu ya wote ikiwa ni washirika. Ama ikiwa mtu huyo ni mfanyakazi tu, kwa maana anafanya kazi juu ya mifugo kwa makubaliano ya ushirika wa matokeo (kama vile kupewa nusu ya mazao au faida), basi mnyama anayekufa hasara yake iko kwa mwenye mali muda wa kuwa mfanyakazi hakufanya uzembe wala kuvuka mipaka. Yeye anakuwa ni mfanyakazi anayechunga, kunywesha na kuhudumia mifugo na hupata kile walichokubaliana, kama nusu au robo ya mazao au faida.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3180/مسالة-في-الشراكة-براس-المال-والجهد
  • Imechapishwa: 31/07/2026