Swali: Kwa nini Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akimtazama mwanamke wa Khath´amiyyah na akageuza uso wa al-Fadhwl? Je, hilo lilikuwa ni jambo lililokuwa halali kwake peke yake au vipi?
Jibu: Hili liko katika mlango wa kujiepusha na sababu za fitina. Kwa sababu kuangalia kunaweza kuwa ni miongoni mwa sababu za fitina, hata kama ni kuangalia umbo au kusikia sauti nzuri; si lazima iwe amefunua uso. Kuhusu mwanamke wa Khath´amiyyah hakuna dalili kwamba alikuwa amefunua uso wake waziwazi. Bali kulikuwa na kuangaliana kati yake na al-Fadhwl, huenda kwa sababu ya mazungumzo au kusikia sauti yake nzuri au sababu nyinginezo. Hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimgeuza uso wa al-Fadhwl kwa kukhofia fitina kwake. Ama Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yeye halikhofiwi hilo kwake, kwa sababu Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amemlinda na fitina kama hiyo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3186/شبهة-توجيه-نظر-رسول-الله-الى-الخثعمية
- Imechapishwa: 01/08/2026
Swali: Kwa nini Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akimtazama mwanamke wa Khath´amiyyah na akageuza uso wa al-Fadhwl? Je, hilo lilikuwa ni jambo lililokuwa halali kwake peke yake au vipi?
Jibu: Hili liko katika mlango wa kujiepusha na sababu za fitina. Kwa sababu kuangalia kunaweza kuwa ni miongoni mwa sababu za fitina, hata kama ni kuangalia umbo au kusikia sauti nzuri; si lazima iwe amefunua uso. Kuhusu mwanamke wa Khath´amiyyah hakuna dalili kwamba alikuwa amefunua uso wake waziwazi. Bali kulikuwa na kuangaliana kati yake na al-Fadhwl, huenda kwa sababu ya mazungumzo au kusikia sauti yake nzuri au sababu nyinginezo. Hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimgeuza uso wa al-Fadhwl kwa kukhofia fitina kwake. Ama Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yeye halikhofiwi hilo kwake, kwa sababu Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amemlinda na fitina kama hiyo.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3186/شبهة-توجيه-نظر-رسول-الله-الى-الخثعمية
Imechapishwa: 01/08/2026
https://firqatunnajia.com/hakuna-dalili-ya-wazi-kwamba-uso-wa-mwanamke-wa-khathamiyyah-ulikuwa-wazi/