Swali: Wote wanajua kuwa Shaykh Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy ni miongoni mwa wanazuoni wakubwa wa Hadiyth na elimu ya wapokezi. Je, hakuzijua dosari zinazodhoofisha Hadiyth ya Asmaa’? Na ni ipi hoja yake katika kuruhusu kufunua uso na mikono?
Jibu: Shaykh Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy ni miongoni mwa ndugu zetu wanaojulikana na anajulikana kwa fadhilah zake na elimu yake. Lakini kama walivyo wanazuoni wengine, anayo makosa na mambo aliyokosea ambayo wanazuoni wanayajua. Hili ni miongoni mwa makosa yake katika Hadiyth hii na katika mambo mengine pia, hata katika suala la Hijaab. Maoni yake ya kuruhusu kufunua uso ni kosa katika hili, kama walivyokosea wengine wakubwa kuliko yeye. Hivyo haipaswi kudhaniwa kuwa fulani au fulani amekingwa na makosa. ash-Shaafi´iy ana makosa, Maalik ana makosa, Ahmad bin Hanbal – nao ni wakubwa kuliko yeye – wana makosa, Abu Haniyfah pia ana makosa na wengineo katika wanazuoni. Kila mwanazuoni ana masuala machache aliyokosea na haki ikamfichika; ama Hadiyth haikumfikia, ilimfikia kwa njia dhaifu au sababu nyinginezo. Hivyo kila mwanazuoni ana makosa na inatosha kwa mtu kuwa na ubora hata kama makosa yake yanahesabiwa, kwani hakuna mtu anayesalimika kabisa na makosa.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3187/توجيه-كلام-الالباني-في-تحسين-حديث-اسماء-في-كشف-الوجه
- Imechapishwa: 01/08/2026
Swali: Wote wanajua kuwa Shaykh Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy ni miongoni mwa wanazuoni wakubwa wa Hadiyth na elimu ya wapokezi. Je, hakuzijua dosari zinazodhoofisha Hadiyth ya Asmaa’? Na ni ipi hoja yake katika kuruhusu kufunua uso na mikono?
Jibu: Shaykh Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy ni miongoni mwa ndugu zetu wanaojulikana na anajulikana kwa fadhilah zake na elimu yake. Lakini kama walivyo wanazuoni wengine, anayo makosa na mambo aliyokosea ambayo wanazuoni wanayajua. Hili ni miongoni mwa makosa yake katika Hadiyth hii na katika mambo mengine pia, hata katika suala la Hijaab. Maoni yake ya kuruhusu kufunua uso ni kosa katika hili, kama walivyokosea wengine wakubwa kuliko yeye. Hivyo haipaswi kudhaniwa kuwa fulani au fulani amekingwa na makosa. ash-Shaafi´iy ana makosa, Maalik ana makosa, Ahmad bin Hanbal – nao ni wakubwa kuliko yeye – wana makosa, Abu Haniyfah pia ana makosa na wengineo katika wanazuoni. Kila mwanazuoni ana masuala machache aliyokosea na haki ikamfichika; ama Hadiyth haikumfikia, ilimfikia kwa njia dhaifu au sababu nyinginezo. Hivyo kila mwanazuoni ana makosa na inatosha kwa mtu kuwa na ubora hata kama makosa yake yanahesabiwa, kwani hakuna mtu anayesalimika kabisa na makosa.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3187/توجيه-كلام-الالباني-في-تحسين-حديث-اسماء-في-كشف-الوجه
Imechapishwa: 01/08/2026
https://firqatunnajia.com/ibn-baaz-kuhusu-maoni-ya-al-albaaniy-kujuzisha-mwanamke-kuonyesha-uso-wake/