Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke kukata sehemu ya nywele zake? Tunaomba ufafanuzi, kwani jambo hili limeenea kwa wanawake wa Kiislamu.
Jibu: Kuziacha nywele kama zilivyo ni bora zaidi, kwa sababu ni uzuri na pambo kwake. Ama kukata nywele, hatujui ubaya wake ikiwa ni kwa ridhaa ya mume wake ikiwa ameolewa na wakakubaliana juu ya hilo, au ikiwa hana mume na akakata nywele zake kwa ajili ya kupunguza uzito wake kutokana na kuwa nyingi – si kwa sababu ya kujifananisha na makafiri wala wanaume – bali kwa ajili ya kupunguza tu, basi hilo halina neno kwa kadiri tunavyojua na haijaja dalili inayokataza hilo. Kilichokuja katika Shari´ah ni kukataza kunyoa kabisa. Ama kukata tu hatujui katazo lake. Wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walipunguza nywele zao baada ya kufariki kwake kwa ajili ya kupunguza uzito, kwani nywele nyingi huwa nzito. Kwa hiyo kupunguza kwa ajili ya haja hiyo hakuna ubaya, lakini kuziacha kama zilivyo kwa ajili ya uzuri, khaswa kwa wanawake vijana, basi hilo ndilo bora na salama zaidi.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3203/حكم-قص-شعر-المراة-للزينة
- Imechapishwa: 01/08/2026
Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke kukata sehemu ya nywele zake? Tunaomba ufafanuzi, kwani jambo hili limeenea kwa wanawake wa Kiislamu.
Jibu: Kuziacha nywele kama zilivyo ni bora zaidi, kwa sababu ni uzuri na pambo kwake. Ama kukata nywele, hatujui ubaya wake ikiwa ni kwa ridhaa ya mume wake ikiwa ameolewa na wakakubaliana juu ya hilo, au ikiwa hana mume na akakata nywele zake kwa ajili ya kupunguza uzito wake kutokana na kuwa nyingi – si kwa sababu ya kujifananisha na makafiri wala wanaume – bali kwa ajili ya kupunguza tu, basi hilo halina neno kwa kadiri tunavyojua na haijaja dalili inayokataza hilo. Kilichokuja katika Shari´ah ni kukataza kunyoa kabisa. Ama kukata tu hatujui katazo lake. Wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walipunguza nywele zao baada ya kufariki kwake kwa ajili ya kupunguza uzito, kwani nywele nyingi huwa nzito. Kwa hiyo kupunguza kwa ajili ya haja hiyo hakuna ubaya, lakini kuziacha kama zilivyo kwa ajili ya uzuri, khaswa kwa wanawake vijana, basi hilo ndilo bora na salama zaidi.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3203/حكم-قص-شعر-المراة-للزينة
Imechapishwa: 01/08/2026
https://firqatunnajia.com/mwanamke-kukata-sehemu-ya-nywele-zake-kwa-ajili-ya-kujipamba/