Swali: Inajuzu kwa baba kumpa matumizi mtoto wake mmoja na asimpe mwengine ikiwa mtoto huyo amepasi kwenye mtihani tofauti na mwengine?

Jibu: Hapana, haijuzu:

“Mcheni Allaah na fanyeni uadilifu kati ya watoto wenu.”[1]

Lakini hata hivyo inafaa akamtofautisha mtoto mmoja kukiwa kuna sababu kama vile mmoja wao ni fakiri. Ampe kwa ajili ya ufakiri wake, na sio kwa ajili ya kumtukuza. Hakuna neno. Hali kadhalika kumpa kwa ajili ya kumlipia deni lake; amtofautishe kwa ajili ya kumlipia deni lake. Hakuna neno.

[1] al-Bukhaariy (2587).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (58) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/15-01-1438-ighastat.mp3
  • Imechapishwa: 27/10/2017