Swali: Nina mama anayevuta sigara. Pindi ninapomkataza kuvuta sigara hunikasirikia, anasababisha matatizo makubwa na anataka kutoka kujinunulia mwenyewe. Ni mgonjwa wa akili. Inajuzu kwangu kumnunulia sigara?

Jibu: Ni maasi:

“Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba.”[1]

Mnasihi na umbainishie madhara ya sigara. Mweleze kuwa ni maasi yasiyojuzu yanayomdhuru yeye na afya yake na pia ni uchafu. Huenda akakinaika na kuacha.

[1] al-Bukhaari (7258) na Muslim (1840).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (8) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–14340429.mp3
  • Imechapishwa: 09/02/2017