Swali: Ikiwa msichana alifanyiwa operesheni kwa mfano tumboni na hilo likapelekea kufanya chale ya upasuaji na kushona na hilo lilitokea wakati wa kuzaliwa au miezi kadhaa baada yake. Akijitokeza anayetaka kumchumbia msichana huyu ni lazima kwa familia yake wamjulishe kuhusu operesheni hii na kwamba iliacha alama mpaka hii leo? Je, hiyo ni haki yake mchumbiaji ki-Shari´ah?
Jibu: Ni lazima kwa muislamu kulazimiana na ukweli katika mambo yake yote. Hakika ukweli ni uokozi na usalama. Ikiwa msichana atajiwa na mchumba na akawa yuko na alama iliyotajwa itokanayo na operesheni hiyo, basi wanapasa kumjuza. Kwa sababu pengine baadhi ya watu wasivumilie na wakakereka na alama hiyo wasipojua. Pengine kukatokea matatizo kati yake yeye na familia yake mwanamke na mwanamme akadai kuwa hiyo ni kasoro kwa mwanamke huyo. Kwa hivyo kinachotakikana kwao ni wao kumjuza mume juu ya hali yake ili awe na utambuzi na wasije kupatwa na majuto baadaye.
- Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/حكم-كشف-عيوب-المرأة-أمام-الخاطب-لها
- Imechapishwa: 12/06/2022
Swali: Ikiwa msichana alifanyiwa operesheni kwa mfano tumboni na hilo likapelekea kufanya chale ya upasuaji na kushona na hilo lilitokea wakati wa kuzaliwa au miezi kadhaa baada yake. Akijitokeza anayetaka kumchumbia msichana huyu ni lazima kwa familia yake wamjulishe kuhusu operesheni hii na kwamba iliacha alama mpaka hii leo? Je, hiyo ni haki yake mchumbiaji ki-Shari´ah?
Jibu: Ni lazima kwa muislamu kulazimiana na ukweli katika mambo yake yote. Hakika ukweli ni uokozi na usalama. Ikiwa msichana atajiwa na mchumba na akawa yuko na alama iliyotajwa itokanayo na operesheni hiyo, basi wanapasa kumjuza. Kwa sababu pengine baadhi ya watu wasivumilie na wakakereka na alama hiyo wasipojua. Pengine kukatokea matatizo kati yake yeye na familia yake mwanamke na mwanamme akadai kuwa hiyo ni kasoro kwa mwanamke huyo. Kwa hivyo kinachotakikana kwao ni wao kumjuza mume juu ya hali yake ili awe na utambuzi na wasije kupatwa na majuto baadaye.
Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/حكم-كشف-عيوب-المرأة-أمام-الخاطب-لها
Imechapishwa: 12/06/2022
https://firqatunnajia.com/kumjuza-mchumbiaji-kovu-litokanalo-na-operesheni/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)