Kumjamii mwanamke mwenye hedhi kwenye tupu ya nyuma

Swali: Umesema kuwa mwanamke mwenye hedhi inajuzu kumjamii mbali na tupu ya mbele. Je, kwa hilo inapata kufahamika kwamba inajuzu kumjamii kwenye tupu ya nyuma?

Jibu: Hapana. Hili ni haramu, ni mamoja kwa mwenye hedhi na asiyekuwa na hedhi. Ni haramu. Hii ni liwati. Ni dhambi kubwa miongoni mwa madhambi makubwa. Anaweza kumjamii kwenye mapaja yake na sehemu nyingine ambazo anaweza kustarehe na akamwaga. Hili limeruhusiwa.

Check Also

Mume kuangalia uchi wa mke wake

Swali: Inajuzu kwa mwanaume kuangalia uchi wa mke wake na ni upi mpaka ulioruhusiwa? Jibu: …