Swali: Ni wanachuoni gani waliobaki baada ya kufa Shaykh al-Albaaniy, Ibn Baaz na Ibn ´Uthaymiyn?

Jibu: Waliobaka ni wengi na himdi zote ni Zake Allaah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikufa na wakabaki Maswahabah zake watukufu. Ahmad bin Hanbal alikufa na wakabaki wenzake. Ibn Taymiyyah alikufa na wakabaki wenzake. Ibn ´Abdil-Wahhaab alikufa na wakabaki wenzake. Kadhalika wamefariki watu hawa na wamebaki wanafunzi zake na ndugu zake wengine. Haki haipotei. ´Umar alipodungwa kisu na akaambiwa achague atayembakilia, alisema:

“Allaah Hakuwa ni mwenye kuipoteza Dini Yake.”

Allaah Hawezi kuipoteza Dini hii kamwe. Ni juu yenu kusimama kidete na kunyanyua bendera ya Sunnah na ya haki.

“Hakutoacha kuwepo kipote katika Ummah wangu kikiwa juu ya haki wazi wazi. Hakitodhuriwa na wenye kuwapinga na kwenda kinyume nao mpaka itapokuja ahadi ya Allaah.”

Elimu haikufa na wanachuoni hawakufa. Himdi zote ni Zake Allaah baraza la wanachuoni wakubwa wana kheri ndani yake na baraka. Kadhalika ndugu zetu Shaam na Yemen. Dunia imejaa wanafunzi wakubwa ambao wanaziba pengo hili. Hivyo watu wa batili wasipeane bishara njema na wala wasifurahi.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaasid Kitaab-ish-Sharï´ah (1/208-209)
  • Imechapishwa: 19/05/2015