Swali: Ni ipi hukumu kwa mwenye kumbusu mke wake akiwa na twahara na anataka kuswali?
Jibu: Hakuna neno juu yake. Akimbusu mke wake na asitokwe na kitu wudhuu´ wake ni sahihi kutokana na maoni yenye nguvu. Wako wanachuoni wenye kuona kuwa kumbusu kunachengua wudhuu´. Wengine wakasema kile kitendo cha kumgusa tu kunachengua wudhuu´. Maoni ya sawa ni kwamba hayachengui wudhuu´. Haya ndio maoni yenye nguvu katika maoni ya wanachuoni kwamba kumgusa mwanamke au kumbusu hakuchengui wudhuu´ kwa sharti asitokwe na kitu; si madhiy wala kitu kingine.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdil-´Aziyz bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3788/هل-تقبيل-الزوجة-ينقض-الوضوء
- Imechapishwa: 05/04/2020
Swali: Ni ipi hukumu kwa mwenye kumbusu mke wake akiwa na twahara na anataka kuswali?
Jibu: Hakuna neno juu yake. Akimbusu mke wake na asitokwe na kitu wudhuu´ wake ni sahihi kutokana na maoni yenye nguvu. Wako wanachuoni wenye kuona kuwa kumbusu kunachengua wudhuu´. Wengine wakasema kile kitendo cha kumgusa tu kunachengua wudhuu´. Maoni ya sawa ni kwamba hayachengui wudhuu´. Haya ndio maoni yenye nguvu katika maoni ya wanachuoni kwamba kumgusa mwanamke au kumbusu hakuchengui wudhuu´ kwa sharti asitokwe na kitu; si madhiy wala kitu kingine.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdil-´Aziyz bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3788/هل-تقبيل-الزوجة-ينقض-الوضوء
Imechapishwa: 05/04/2020
https://firqatunnajia.com/kumbusu-mke-baada-ya-kutawadha-kunachengua-wudhuu/