Kulipa deni kwa pesa nyingine 1

Swali: Miaka mitatu iliyopita nilikopa 10.000$. Hivi sasa nataka kulipa deni hilo kwa fedha nyingine. Alonipa deni lile anataka nimlipe kwa thamani ya pesa ya leo na sio kwa thamani ile ile iliokuwa miaka mitatu iliyopita…

Jibu: Mambo ni hivyo. Inatakiwa iwe kwa thamani ya sasa, kwani ndipo deni limelipwa.

Swali: Kama unavyojua dola imepanda kiasi kikubwa jambo ambalo linanidhuru. Ni wajibu kwangu kufanya hivo?

Jibu: Unatakiwa kulipa kile ulichokopa kwake hata kama thamani imepanda. Unatakiwa kulipa pesa ile ile iliyoazima kwake katika dola au pesa nyingine. Haijalishi kitu hata kama thaman yake imepanda. Hii ni haki yake ilio katika dhimma yako.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (58) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/15-01-1438-ighastat.mp3
  • Imechapishwa: 01/04/2017