Kuswali na nguo zilizotengenezwa na ngozi ya wanyama wakali

Swali: Inajuzu kuvaa nguo zilizotengenezwa na ngozi ya wanyama nyamafu wakali?

Jibu: Hapana, haijuzu. Haijuzu kuvaa ngozi ya wanyama wakali, kukaa juu yake wala kuzitumia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza hilo.

Swali: Akiswali amezivaa swalah yake ni sahihi?

Jibu: Maadamu amefunika viungo vyake vya siri swalah yake ni sahihi pamoja na uharamu na dhambi, ni kama nguo ilioibwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (9) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–14340506.mp3
  • Imechapishwa: 02/04/2017