Swali: Wapo vijana wengi ambao ni wepya na wako tayari kuwanufaisha watu ni mamoja misikitini au maeneo ya umma. Wanauliza kama inafaa kwao kuwalingania watu wanaohitajia Qur-aan na Sunnah au kwanza wapate idhini kutoka serikalini?

Jibu: Naona kuwa haifai kwao wakazungumza kwa yale mambo waliyokatazwa kuzungumza isipokuwa kwa idhini. Ni lazima kumtii mtawala inapokuja katika upangiliaji wa mambo. Wewe mwenyewe unajua endapo wadogo na wanafunzi wepya wataidhinishwa watasema mambo wasiyoyajua. Jambo hilo litapelekea katika madhara. Watu watachanganyikiwa. Mambo yanaweza kupelekea mpaka katika ´Aqiydah, sembuse matendo ´ibaadah za kimatendo. Makatazo hayo kutoka serikalini sio makatazo ya moja kwa moja mpaka tuseme kwamba mtawala hatakiwi kutiiwa katika jambo hilo, kwa sababu makatazo hayo yanazuia kufikishwa kwa Shari´ah. Makatazo hayo ni yenye kufupizika na malengo ni kujua ni yupi anastahiki kufanya hivo na ni yupi asiyestahiki. Kama mnavojua mwenyewe ni kwamba serikali inampa kibali kila mwenye kuomba ambaye anastahiki. Hatutambui kwamba wamemzuia yeyote ambaye anastahiki kueneza elimu. Jambo hili linampa utulivu mtu. Haijuzu kwa yeyote kuzungumza katika maeneo ambayo imekatazwa kuzungumza, kama vile msikitini au maeneo ya umma, isipokuwa baada ya idhini kutoka kwa mtawala. Hata hivyo inafaa kwake kuzungumza na ndugu zake kama kwa mfano chumbani mwake. Hakuna yeyote anayekatazwa kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (10 A)
  • Imechapishwa: 01/09/2021