Malaika mwingine ni yule ambaye amepewa kazi ya kupuliza baragumu. Malaika huyo anaitwa Israafiyl. Atakapopuliza mara ya kwanza kwenye baragumu basi watazimia na kufa wale wote walioko mbinguni na ardhini. Atakapopuliza mara ya pili watapata uhai kwa mara nyingine. Huu ni upulizaji wa Kufufuliwa. Amesema (Ta´ala):

وَنُفِخَ فِي الصُّورِ فَصَعِقَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ إِلَّا مَن شَاءَ اللَّـهُ ۖ ثُمَّ نُفِخَ فِيهِ أُخْرَىٰ فَإِذَا هُمْ قِيَامٌ يَنظُرُونَ

“Itapulizwa katika baragumu, basi watazimia wale walioko mbinguni na ardhini isipokua amtakaye Allaah. Kisha litapulizwa humo jengine, tahamaki hao wanasimama wakitazama.”[1]

[1] 39:68

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 81
  • Imechapishwa: 01/09/2021