Jibriyl (´alayhis-Salaam) amepewa kazi ya kufikisha Wahy, Mikaaiyl (´alayhis-Salaam) amepewa kazi ya kushughulikia mvua. Malaika wengine ni wenye kutekeleza maamrisho ya Allaah mbinguni na ardhini. Pale ambapo Allaah anaamrisha jambo basi Malaika upesi wanateremka nayo pale alipotaka na wanaitekeleza kwa viumbe. Kila Malaika miongoni mwao anayo kazi yake maalum.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 81
  • Imechapishwa: 01/09/2021