Kuleta nyuradi zinazodi juu ya kile kilichopokelewa

Swali: Ikiwa mtu ana kawaida ya kuleta nyiradi kila siku baada ya Fajr na baada ya Maghrib kutoka katika Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – je, kuna ubaya wowote katika hilo hata kama haikupokewa moja kwa moja? Kwa maana ya kwamba ameongeza juu ya yale yaliyopokelewa katika Kitabu cha Allaah na Sunnah Swahiyh?

Jibu: Ikiwa ameongeza katika Dhikr na du´aa, hakuna tatizo. Akijitahidi kufuata yale yaliyopokelewa na kuongeza juu yake, ndio bora zaidi. Ila kama ataongeza du´aa kutoka kwake mwenyewe kwa haja aliyonayo au maneno ya Dhikr ambayo hayajapokelewa, basi hakuna ubaya. Mfano kama kusema:

سبحان الله العظيم الجليل القدوس الملك الرحمن، سبحان الله العظيم الشأن، سبحان الله القادر على كل شيء

”Allaah ametakasika kutokana na mapungufu, Mtukufu, Mwingi wa kutakasika, Mfalme na Mwingi wa rehema. Allaah ametakasika kutokana na mapungufu, Mwenye shani kubwa. ”Allaah ametakasika kutokana na mapungufu, Muweza juu ya kil jambo.”.

Hata kama hayakupokelewa katika Hadiyth, hakuna tatizo. Kwa sababu yote ni tasbihi na utakasifu.

Swali: Kama atatumia Dhikr hii ya kila siku kwa ajili ya matabano na ikaonyesha manufaa katika kuponya baadhi ya maradhi – je, anaweza kuendelea nayo bila tatizo?

Jibu: Hakuna neno. Sioni tatizo lolote katika hilo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31174/حكم-الذكر-والدعاء-الزاىد-عن-الكتاب-والسنة
  • Imechapishwa: 08/10/2025