Tatizo kwa dada huyu muulizaji ni kwamba amesema kuwa ana wavulana wawili ambao hawaswali. Hili ni tatizo kubwa kabisa. Ikiwa hawaswali kabisa, si msikitini wala nyumbani, basi wote wawili ni makafiri. Wakiwa wamekwishabaleghe na ni wenye akili. Kwa sababu kuacha swalah ni kufuru kubwa inayomtoa mtu nje ya Uislamu. Kwa kuthibitisha hilo tumetunga kitabu kidogo lakini chenye maana kubwa ambapo ndani yake tumebainisha dalili kutoka katika Qur-aan, Sunnah na maneno ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) juu ya kwamba kuacha swalah moja kwa moja ni kufuru inayomtoa mtu nje ya Uislamu. Mwenye kufanya hivo anazingatiwa ni mwenye kuritadi. Akirudi katika Uislamu na akaanza kuswali, basi hilo ndilo linalotakikana. Asiporudi basi ni wajibu kwa mtawala kumuua. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kubadilisha dini yake basi muueni.”

Lakini Allaah hajafunga mlango wa kutubia. Mlango wa kutubia umefunguliwa. Ni wajibu kwa yule aliyeacha swalah atubie kwa Allaah. Zile swalah zilizopita alizoacha sio lazima kuzilipa. Lakini anatakiwa kuanza kuanzia mwanzo na aswali. Tawbah inafuta yaliyotangulia, kama alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Nataraji kutoka kwa mwanamke huyu, bali nataraji kutoka kwa baba mwenye watoto hawa awashughulikie watoto hawa wawili ambao haswali.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (58) http://binothaimeen.net/content/1316
  • Imechapishwa: 28/10/2019