Kulala au kupumzika kabla ya kufanya ´Umrah

Swali: Ni ipi hukumu ya ambaye amefika Makkah kisha akachelewesha kufanya ´Umrah kwa muda wa masaa kadhaa ili aweze kulala, kupumzika au kula?

Jibu: Hakuna neno hata kama ni kwa masiku kadhaa. Hata hivyo anatakiwa kubaki katika Ihraam yake, asitoke kwenye Ihraam yake au akafanya jambo lililokatazwa. Anatakiwa kulazimiana na Ihraam yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (24) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdatul-20-02-1435.mp3
  • Imechapishwa: 27/07/2020