Swali: Kuna mtindo umeenea mahala kunaposwaliwa ´iyd ambapo kunagawanywa tende kabla ya swalah ili watu wapate fadhilah za tende. Je, hichi ni kitendo cha Sunnah au kimezushwa?

Jibu: Huu ni mwenendo wa vijana – Allaah awaongoze. Salaf hawakuwa wanafanya hivi. Hatujui kuwa walikuwa wanagawa tende katika uwanja wa kuswalia. Lililothibiti ni kuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anakula tende kabla ya kutoka nyumbani kwake. Yule anayetaka kufanyia kazi Sunnah ale kabla ya kutoka nyumbani kwake na si kula msikitini.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_07.mp3
  • Imechapishwa: 30/07/2020