Kula tende msikitini siku ya idi

Swali: Kuna mtindo umeenea mahala kunaposwaliwa Idi ambapo kunagawiwa tende kabla ya Swalah ili watu wapate fadhila za tende. Je, hichi ni kitendo cha Sunnah au kimezushwa?

Jibu: Huu ni mwenendo wa vijana – Allaah Awaongoze. Salaf hawakuwa wanafanya hivi. Hatujui kuwa walikuwa wanagawa tende mahala pa kuswalia. Lililothibiti ni kuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anakula tende kabla ya kutoka nyumbani kwake. Yule anayetaka kufanyia kazi Sunnah ale kabla ya kutoka nyumbani kwake na si kula Msikitini.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (07) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_07.mp3
  • Imechapishwa: 01/06/2015