Kukusanyika kusoma Qur-aan kwa ajili ya kupata baraka kazini

Swali: Je, inajuzu kwa mtu kuwakusanya watu na akawaamrisha kumsomea Qur-aan kwa lengo moja wapo kama mfano wa kubadilisha kazi na akawakusanya watu wamsomee Qur-aan ili aweze kufikiwa na baraka katika kazi yake?

Jibu: Allaah ameteremsha Qur-aan ili watu waabudu kwa kisomo chake na kutendea kazi hukumu zake na iwe ni miujiza kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kitendo hichi ulichotaja sio miongoni mwa mambo yaliyoweka Allaah (Subhaanah).

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/343)
  • Imechapishwa: 23/08/2020