Swali: Baadhi ya watu wanakuwa na nguo pana na wanapotaka kusujudu wanaisokota ili asiiketie aliyeko kuliani au kushotoni.

Jibu: Hilo halidhuru. Huyu amesujudia juu yake.

Swali: Makatazo ya kukunja nguo ni ili asisujudie juu yake?

Jibu: Huyu hakuacha kusujudia juu yake. Amesujudu juu yake. Amefanya hivo ili asiwaudhi wengine au akaudhika yeye mwenyewe.

Swali: Vipi kukunja nywele na kuweka kilemba nyuma ya mgongo?

Jibu: Ndio. Akiache kilemba kama kilivyo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23772/ما-حكم-كف-الثوب-والشعر-في-الصلاة
  • Imechapishwa: 25/04/2024