Swali: Mwadhini alichelewa kidogo wakati wa adhaana ambapo akaadhini mmoja katika ndugu walioko msikitini. Wakati wa kukimu akakimu yule mwadhini ambaye ni mteule msikitini. Je, kuna ubaya kwa kufanya hivo? Namaanisha kwamba inafaa akatoa adhaana mmoja akakimu mwengine?

Jibu: Hapana vibaya kufanya hivo. Lakini bora ni akimu ambaye ameadhini. Hivo ndivo ilivyokuwa hali wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Imepokelewa kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amesema:

“Mwenye kuadhini ndiye hukimu.”[1]

Lakini cheni ya wapokezi wake ni dhaifu.

[1] at-Tirmidhiy (199), Abu Daawuud (514), Ibn Maajah (717) na Ahmad (04/169).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/339)
  • Imechapishwa: 18/09/2021