Kujitoa muhanga ni kujiua na haijuzu

Swali: Je, ambaye anajilipua anazingatiwa amejiua nafsi yake?

Jibu: Hapana shaka. Kujiua ambako kunaitwa kujitoa muhanga ni kujiua. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَمْوَاتًا ۚ بَلْ أَحْيَاءٌ عِندَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ

“Usifikirie kabisa wale waliouawa katika njia ya Allaah ni wafu. Bali wahai kwa Mola wao wanaruzukiwa.”[1]

Hakusema ”wale wanaoziua nafsi zao”. Haijuzu kwa mtu kujiua nafsi yake kwa hali yoyote na kusema eti ni jihaad. Haijuzu.

[1] 03:169

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (45)
  • Imechapishwa: 26/07/2024