Ni sahihi kufanya sababu za tahadhari kwa sababu ya kujilinda, khaswa inapohusiana na swalah za ´iyd mbili, swalah tano na swalah ya ijumaa. Ni lazima wajiweke mbali kwa ajili ya kuepuka maambukizi. Kuwepo kati ya watu wawili upenyo. Mbali na minasaba hii kilichowekwa katika Shari´ah ni waswaliji waswali kwa kusongamana na wasiache upenyo kwa ajili ya shaytwaan. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Zitengenezeni safu zenu. Zitengenezeni safu zenu. Zitengenezeni safu zenu. Napaa kwa Allaah! Ima mzitengeneze safu zenu au Allaah atazifarikisha nyoyo zenu.”[1]

Ni lazima kwa waislamu kuyazingatia haya. Kujitenga huku kwa jamii ni kwa muda tu na baada ya hapo watarudi katika yale aliyowawekea Allaah Shari´ah kwa njia ya kuzibananisha safu zao.

[1] al-Albaaniy amesema:

”Ameipokea Abu Daawuud (662), Ibn Hibbaan (396), Ahmad (4/276) na ad-Duulaabiy (2/86).” (Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (1/1/72) )

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=fC1jDZ0lO3k
  • Imechapishwa: 20/08/2021