Usingizi unaochengua wudhuu´ na usiochengua

Swali: Pindi ninaposwali Dhuhaa na nikasubiri Dhuhr huzidiwa na ulalaji. Je, wudhuu´ wangu unachenguka?

Jibu: Kusinzia hakuchengui wudhuu´. Kinachochengua ni kulala ambako mtu hahisi yanayoendelea pambizoni mwake. Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) kipindi cha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa wanasubiri ´Ishaa ambapo vichwa vyao vinainama kutokana na kusinzia kisha wanainuka na wala hawatawadhi. Kuhusu usingizi mzito ambao unaondosha hisia unachengua wudhuu´. Kwa hivyo, ee dada kwa ajili ya Allaah, unatakiwa kutambua tofauti kati ya usingizi mzito unaoondosha zile hisia na kulala.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/142)
  • Imechapishwa: 20/08/2021