Swali: Kuna mtu amejiharamishia kula kitu kilichochumwa na mikono ya mwengine. Je, atoe kafara?

Jibu: Masuala haya yanahusiana na kuharamisha kile alichohalalisha Allaah. Allaah ametujibia nayo kwa kusema:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ لِمَ تُحَرِّمُ مَا أَحَلَّ اللَّـهُ لَكَ ۖ تَبْتَغِي مَرْضَاتَ أَزْوَاجِكَ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ قَدْ فَرَضَ اللَّـهُ لَكُمْ تَحِلَّةَ أَيْمَانِكُمْ

“Ee Nabii! Kwanini unaharamisha kile alichokuhalalishia Allaah? Unataka kuwaridhisha wake zako na Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu. Allaah amekwishakufaridhishieni ukomboaji kwa viapo vyenu.”[1]

Allaah akafanya kuhalalisha kilicho halali kuwa ni kiapo. Kwa hivyo pindi mtu anapojiharamishia juu ya nafsi yake kitu kwa maana ya kwamba alichokuwa anakusudia ni kujizuia nacho kwa kutumia tamko kama hili, basi hapo atakuwa kwa manzilah ya mwapaji. Inafaa kwake kufanya kile alichoharamisha kisha atoe kafara ya kiapo. Kafara ya kiapo ni kulisha masikini kumi katika chakula cha kawaida tunachowalisha familia zetu, kuwavisha au kuacha mtumwa huru. Asiyeweza hayo basi afunge siku tatu.

[1] 66:01-02

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (19) http://binothaimeen.net/content/13568
  • Imechapishwa: 15/09/2021