Kuingiza vidole kinywani wakati wa kutawadha

Swali: Vipi kuhusu kuingiza vidole kinywani wakati wa kusukutua mdomo?

Jibu: Hapana, si lazima. Inatosa kusukutua mdomo. Wakati wa kusafisha meno atumie Siwaak au kwa kidole chake. Kufanya hivo ndio bora. Si lazima kuingiza vidole. Inatosha akiingiza maji kinywani kisha akayatema.

Swali: Je, anaweka vidole vya kulia au vya kushoto mdomoni?

Jibu: Vya kushoto na Allaah akubariki. Kwa sababu ni kuondosha uchafu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24722/حكم-ادخال-الاصبع-في-الفم-عند-المضمضة
  • Imechapishwa: 02/12/2024