Shaykh Swaalih Aalush-Shaykh: Wakati wa kongamano nilizungumza na Shaykh ´Abdur-Rahmaan [´Abdul-Khaaliq]. Nilifanya muhadhara na nikaulizwa swali kuhusu hukumu ya kuingia bungeni katika nchi ambayo inahukumu kinyume na Shari´ah ya Allaah au inakubali shirki nchini. Jawabu langu likawa kwamba ni lazima kujitenga mbali na washirikina na kwamba kuingia nao katika jambo hilo maana yake ni kwamba mtu amekubaliana kujiunga na kutunga kanuni za nchi zilizosimama katika misingi hiyo. Nikazungumzia kidogo maudhui hayo mpaka nilipomaliza. Shaykh ´Abdur-Rahmaan akazungumza nami juu ya maudhui hayo na akanikasirikia na akasema kuwa yeye amewauliza wanachuoni wakubwa…

Imaam al-Albaaniy: Alizungumza nawe baina yako wewe na yeye au ilikuwa mbele za watu?

Shaykh Swaalih Aalush-Shaykh: Mbele ya kijikundi cha watu maalum ambacho kilikuwa na watu takriban kumi.

Imaam al-Albaaniy: Ina maana haikuwa mbele za watu wote baada ya kalima uliyotoa.

Shaykh Swaalih Aalush-Shaykh: Ilikuwa baada ya kalima yangu lakini si mbele za watu wote. Kwa sababu tuliondoka mahala pale.

Imaam al-Albaaniy: Sawa.

Shaykh Swaalih Aalush-Shaykh: Nikamwambia kwamba jambo hilo ni Ikhwaaniyyah na si kitu kinachotambulika kwa Salafiyyah.

Imaam al-Albaaniy: Kweli.

Shaykh Swaalih Aalush-Shaykh: Ndipo akasema:

“Kwani jambo hilo haiwezi kuwa ile haki walionayo al-Ikhwaan? Ina maana kwamba al-Ikhwaan hawapatii hata siku moja?”

Imaam al-Albaaniy: Mm…

 Shaykh Swaalih Aalush-Shaykh: Ndipo akasema: [Akasema:]

“Ikiwa hii ni haki kwa al-Ikhwaan basi sisi tunaikubali.”

Imaam al-Albaaniy: Mm…

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (1003)
  • Imechapishwa: 06/04/2020